5/11/16

Waandishi wa habari kutoka taasisi ya Malaria no More watembelea Jiji la Arusha.


Mtoto Derick Simon akifanyiwa vipimo vya malaria na mtoa huduma katika zahanati ya Kijenge iliyopo jijini Arusha wakati wa ziara ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.

Edisa Petro akijaza fomu ya kukubali kufanya mahojiano na waandishi wa Habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea zahanati ya Kijenge jijjini Arusha, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria. Katikati ni mwandishi wa habari Luis Velarde.

Bariki Sirimu Ayo akifanya vipimo katika maabara ya kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A to Z jijini Arusha ili kujua ubora wa chandarua kiliyotengenezwa kama kimefikia viwango vinavyotakiwa tayari kwa matumizi. Kushoto ni mfanyakazi kiwandani humo Grace Bayo.

Meneja uzalishaji kiwanda cha kutengenezea vyandarua cha A to Z cha Arusha Binesh Haria akiwaonesha baadhi ya waandishi wa Habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani sampuri za malighafi ya kutengenezea chandarua walipotembelea kiwanda hicho kujionea namna vyandarua vinavyotengenezwa, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria. Kulia ni mwandishi wa habari David Gurien.

Hatua mbalimbali za utengenezaji wa vyandarua katika vyandarua cha A to Z cha jijini Arusha.
Wafanyakazi kiwanda cha kutengenezea vyandarua cha A to Z cha Arusha Grace Bayo (kushoto) na Witness Joseph (kulia) wakihakiki vipimo vya chandarua tayari kupelekwa sokoni kwa watumiaji.

Meneja wa Mawasiliano Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Dena Gudaitis (aliyetangulia) akiwasili kiwanda cha kutengenezea vyandarua cha A to Z cha Arusha kujionea namna vyandarua vinavyotengenezwa, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria. Kulia ni Meneja Utawala na Fedha wa kiwanda hicho Kalpesh Shar na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwasisi wa Taasisi ya Malaria no More Martin Edlund.

Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ziara waliyofanya katika zahanati ya Kijenge jijini Arusha.
(Picha na Eleuteri Mangi, Arusha)
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts