Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/1/16

Wadau wa michezo waombwa kuendelea kujitokeza na kuwekeza katika mchezo wa Riadha


Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim (katikati) jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 jana jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akiwapungia mkono washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim na kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe.

Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18. Katikati ni Katibu wa Naibu Waziri Bibi. Anna Nkinda.

Makamu wa Raisi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. William Kallaghe akisoma taarifa fupi juu ya mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 mbele ya Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(kulia mwenye miwani) jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 kutoka nchi mbalimbali wakipita mbele ya Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(hayupo pichani) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wapili kushoto) akiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18  jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe,Raisi wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha  Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo upande wa Miundombinu Alex Nkenyenge.

Washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 kutoka nchi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati wa  hafla ya ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akimpongeza mmoja wa washiriki kutoka Tanzania ambao wamekuwa washindi wa kwanza kwa wanawake  mbio za relay mita mia nne mara nne alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka18 jana jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akimvalisha medali mmoja wa washiriki kutoka Kenya ambao wamekuwa washindi wa kwanza kwa wanaume mbio za relay mita mia nne mara nne  alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 jana jijini Dar es Salaam.


Mshindi wa kwanza wa mbio za mita 200 katika mashindano ya Afrika Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 Bw. Ally Khamis Ibrahim kutoka Zanzibar ( katikati) na akiwa katika jukwaa moja na washindi wa pili na watatu ambao wate wanatokea nchini Kenya.

Washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 18 kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mashindano hayo kufunga rasmi jana jijini Dar es Salaam.

Picha na Frank Shija