5/13/16

Wafungwa 48 Tanga Kurejeshwa Ethiopia

 
Wafungwa 48 kutoka Ethiopia waliokuwa wanatumikia adhabu kutokana na kuingia nchini bila vibali, wanatarajiwa kurudishwa nchini kwao baada ya kumaliza adhabu hizo.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Andrew Kalengo alisema jana wakati akitoa taarifa ya wahamiaji haramu ya Aprili, mwaka huu kuwa, watu hao wanatarajiwa kupelekwa kwao kwenda kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Alisema watu hao ambao mpaka sasa wapo katika Gereza la Maweni wanasubiri utaratibu wa kurudishwa nchini humo unaoendelea kufanya na Serikali.
Kalengo alisema Idara ya Uhamiaji mkoani hapa imekuwa ikikabiliwa na wimbi kubwa la wahamiaji kutoka nchini humo kutokana na Horohoro kuwa jirani na mpaka unaozitenganisha nchi za Kenya na Tanzania.
“Kuna bandari bubu 48 wanazozitumia wahamiaji hawa, hivyo ni changamoto kulingana na uhaba wa watumishi tulionao,” alisema Kalengo.
Pia, alisema kuna tatizo la ukosefu wa vifaa na uhaba wa watumishi, mambo ambayo ni kikwazo kinachosababisha utendaji kazi wa idara hiyo kutokwenda ipasavyo na kwamba, jamii imekuwa ikitoa msaada kufanikisha malengo yao.
Alisema kati ya Aprili hadi sasa, idara hiyo imezirudisha kaya 20 nchini Kenya zilizokuwa zikiishi kama wahamiaji walowezi kwenye vijiji vya Wilaya ya Mkinga ambayo inapakana na Kenya.
“Katika kipindi cha mwezi Aprili pia tumekamata wahamiaji 14 ambao hawakuwa na kibali cha kuingia nchini kati yao 10 wanatoka Ethiopia, wawili kutoka Kenya, mmoja kutoka India na mwingine Korea Kusini,” alisema.
Kalengo aliwataka Watanzania kutowahifadhi watu wasiowajua, badala yake wawe wepesi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts