5/6/16

Walimu wapewa mkong’oto

 
Walimu watano wamepigwa na kung’olewa mazao yao mashambani na wanakijiji kwa madai  ya kuwazuia kuchungia mifugo katika maeneo ya shule.
Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) wilayani hapa, Baraka Owawa amewaambia waandishi wa habari baada ya kutokea tukio la kati shule za msingi Giriku, Nkindwabiye, Sapiwi na Nyamikoma.
Owawa amewataja walimu waliopigwa na wananchi kwa madai ya kuzuia mifungo kufanya malisho katika maeneo ya shule kuwa ni Masumbuko Jackson, George Mwakanusya, Joseph Marco, Zacharia Jeremiah na Hipolitus Domisian ambao walilazimika kukimbia vituo vyao vya kazi.
Amesema licha ya kupigwa, walimu hao wamepewa vitisho na wanakijiji wanaojiita wazawa kuwa wanaweza kusingiziwa kuwabaka wanafunzi au kutembea na wake za watu ili kuhalalishiwa tuhuma za kuwapiga.

Chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts