5/27/16

Walimu wastaafu wapewa mabati 240

 
Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Mvomero, kimewakabidhi walimu wastaafu 13 mabati 20 kila mmoja kama shukrani kwa kipindi ambacho wamefanya kazi serikalini.
Akizungungumza ofisini kwake baada ya kukabidhi mabati 240 kwa walimu hao, Katibu wa CWT wa wilaya hiyo, Fortunatus Mdengera amesema hiyo ni awamu ya kwanza ya walimu 27 waliostaafu mwaka huu ambao wote watapata mabati 540.
“Kipindi hiki walimu 12 kutoka shule mbalimbali waliostaafu wamepewa mabati 20 kila mmoja,” amesema katibu huyo.
Mdengera amelaani kitendo cha Serikali kuchelewesha malipo ya wastaafu yanayohusu usafiri wa familia na mali zao kurejea katika makazi yao ya asili kama walivyoandika katika mikataba yao aya ajira.
Alisema walimu wote 27 ambao wamestafu katika wilaya hiyohawajalipwa malipo ya kusafirisha mizigo na familia zao hadi leo.
Katibu wa CWT Mkoa wa Morogoro, Issah Ngayama amewataka wastaafu hao kutumia vyema mafao yao baada ya kustaafu ili kuendesha maisha yao vizuri baada ya kuacha kupokea mishahara.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts