Walioachishwa NIDA Kulipwa Mafao | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/22/16

Walioachishwa NIDA Kulipwa Mafao

WATUMISHI 597 wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), waliosimamishwa kazi, Februari mwaka huu, wataanza kulipwa hivi karibuni baada taratibu za malipo kukamilka.
Hayo ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa NIDA, Rose Mdami wakati akizungumza na Nipashe iliyotaka kufahamu mchakato wa ulipwaji fedha watumishi hao baada ya Wizara ya Fedha na Mipango, kuipatia fedha mamlaka hiyo Sh. billioni 2.3.

"Tulipokea barua kutoka wizarani ya malipo hayo ya fedha, taratibu zinaendelea zitakapokamilika hivi karibuni tutaanza kuwalipa watumishi hao," alisema Mdami.

Aidha, kati ya watumishi hao, watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar waliohakikiwa na wizara ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao baada ya kusitishiwa mikataba yao ya kazi.

Watumishi wengine 121 baada ya kuhakikiwa walibainika kuwa na kasoro ikiwamo kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika ofisi ya mwajiri pamoja na kukosekana kwa majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini.

Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja, iliyotolewa wiki iliyopita, ilisema malipo hayo yanahusisha mishahara ya miezi minne, ikiwamo mshahara wa mwezi mmoja baada ya kupatiwa notisi ya kusimamishwa kazi.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa malipo mengine ni pamoja na malimbikizo ya madeni katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Kabla ya fedha hizi kulipwa ulifanyika uhakiki uliohusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali katika majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba za akaunti zilizokuwa zikitumika kulipia mishahara,” alisema Mwaipaja.

NIDA, ilisitisha mikataba ya wafanyakazi wa muda 597 na kubaki na wafanyakazi wakudumu 802 wanaoendelea kufanyakazi huku Kaimu Mkurugenzi wa NIDA Modestus Kipilimba, akisema kuwa kusitishakwa mikataba ya wafanyakazi 597 kulitokana mamlaka hiyo kukabiliwa na ukata wa fedha kwa ajili ya kuwalipa mishahara.

google+

linkedin