5/29/16

Waliohamishwa kupisha Upanuzi wa Uwanja wa ndege 2012 wameendelea kulalamikaWakazi 174 kati ya 864 waliohamishwa na halmashauri ya manispaa Ilala kupisha Upanuzi wa Uwanja wa ndege mwaka 2012 wameendelea kulalamikia manispaa ya Ilala kwa madai ya kuwapatia viwanja hewa 174 ambayo wamiliki wa meneo hayo wamegoma kuwaruhusu kuingia kwa madai kuwa hawajalipwa fidia mashamba hayo.

Wakazi hao waliopelekwa katika viwanja hivyo vilivyopimwa katika maeneo ya Pugu kinyamwezi,Kigogo fresh,zavala na Nyeburu wamesema pamoja na kukabidhiwa hati za umiliki wa maeneo waliyopelekwa baada ya nyumba zao kuvunjwa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege lakini wamiliki wamegoma kuachia maeneo hayo kwa madai ya kutolipwa fidia .

Wakizungumza na chanel ten ambayo ilitembelea maeneo hayo yenye Mgogoro wananchi hao wakiongozwa na kamati ya wananchi walioondolewa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege,wamesema mpaka sasa wamekuwa katika maisha ya shida huku mamlaka zinazohusika zikishindwa kuingilia kati mgogoro huo.

Aidha wakazi hao wamedai kuwa baadhi yao walipewa viwanja vilivyoitwa alama T ,lakini walipotaka Kuviendelea walielezwa kuwa maeneo hayo ni ya wazi ambayo ni ya huduma za kijamii ikiwemo ya Makaburi,shule zahanati na viwanja vya wazi na kubaki njia panda na kumuomba Mkuu wa mkoa wa dsm paul makonda kuingilia kati baada ya kudai manispaa ya ilala imeshindwa kutatua mgogoro huo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts