5/2/16

Wanafunzi Wageuziana Migongo Darasani


Wanafunzi 218 wa kuanzia darasa la tatu hadi la sita katika Shule ya Msingi Zawa, Kata ya Mwang’honoli wilayani hapa, Mkoa wa Simiyu wanasoma katika vyumba viwili vya madarasa kwa kugeuziana migongo.


Hayo yalisemwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ramadhan Kitundumbele mbele ya waandishi wa habari waliotembelea shule hiyo kuangalia changamoto zinazoikabili.


Alisema wanafunzi 59 wa darasa la tatu na 54 wa darasa la nne wanasoma katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo, huku wanafunzi 53 wa darasa la tano na 52 wa la sita wakisomea katika chumba kimoja kimoja kwa kugeuziana migongo.


Ofisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Maswa, Simon Bujimu alisema jitihada zinafanyika ikiwamo kupitia wadau mbalimbali wa elimu kukabiliana na changamoto hizo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm