5/5/16

Wanaolipa Mishahara Chnini ya Kima Kufuatiliwa.MKUU WA MKOA WA MOROGORO BWANA KEBWE STEVEN KEBWE AMEWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUFUATILIA KWA UKARIBU MAJINA YA WAAJIRI WANAOLIPA MISHAHARA CHINI YA KIMA CHA SERIKALI ILI WACHUKULIWE HATUA
AKIZUNGUMZA KATIKA KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI ILIYOFANYIKA KIMKOA MJINI IFAKARA WILAYA YA KILOMBERO BW. KEBWE ALISISITIZA VIONGOZI NA WAFANYAKAZI KUWAWAJIBISHA WAAJIRI WA NAMNA HIYO WANAOKWENDA KINYUME NA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI.
AIDHA ALIONGEZA KUWA CHANGAMOTO YA MISHAHARA DUNI YA WATUMISHI WA SERIKALI ATAWASILISHA KATIKA NGAZI YA TAIFA ILI IFANYIWE KAZI NA WAFANYAKAZI  WALIPWE MSHAHARA UTAKAOPUNGUZA MATATIZO YAO.
ALIONGEZA KUWA AMEPOKEA CHANGAMOTO YA WATUMISHI KUCHELEWA KUPANDISHWA VYEO NA KUWATAKA WATUMISHI KUTAMBUA KUWA SUALA HILO LIPO KISHERIA NA KUWATAKA WAAJIRI KUWAPANDISHA VYEO WAAJIRIWA WENYE SIFA ZA KUPANDA VYEO.
SHEREHE HIZO ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA ZIMEBEBA KAULI MBIUO ISEMAYO “DHANA YA MABADILIKO ILENGE KUINUA HALI YA WANYAKAZI” 

chanzo: http://www.ulangadc.go.tz
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts