5/28/16

‘Wanaume Wenye Korodani Zisizoshuka Hatarini’


Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya stori kubwa ni hii ya gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Wanaume wenye korodani zisizoshuka hatarini’, Gazeti hilo limeripoti kuwa wanaume ambao korodani zao hazijashuka kwenye mfuko wake wapo hatarini kwani kuna uwezekano mkubwa wa kugeuka kuwa saratani zikiwa tumboni.
Gazeti hilo lilifanya mahojiano na Daktari Bingwa wa Mfumo wa Njia ya Mkojo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ‘MNH’ Ryuba Nyamsogoro ambapo aliyazungumza haya………
>>>’kawaida mwanaume ana korodani mbili, moja ikiwa upande wa kushoto na nyingine upande wake wa kulia. Huwa zinatengenezewa tumboni na baadae hushuka hadi katika vifuko vyake vilivyoko nje ya mwili wa mwanaume karibu na uume
Daktari alieleza sababu mbalimbali ambazo huweza kuchangia hali hiyo ikiwamo mtoto kuzaliwa akiwa hajatimiza muda wake (njiti), pacha au kuzaliwa akiwa na upungufu wa homoni ya androgen.
Daktari huyo aliongeza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa katika vizazi hai 100 vya watoto wa kiume kila mwaka ulimwenguni wanne huzaliwa wakiwa na tatizo hilo.
>>>’Kwa hapa nchini bado hatuna takwimu halisi za hali ilivyo lakini hapa muhimbili tumekua tukipokea takribani watoto wanne wenye tatizo la korodani kutoshuka na kuwafanyia upasuaji’ :- Daktari
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts