Wasanii wa Injili wanufaika na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/9/16

Wasanii wa Injili wanufaika na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)


Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu akizindua kujiunga kwa wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) katika huduma ya Bima ya Afya kutoka kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho Askofu Dkt. Rejoyce Ndalima,Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Addo November, Meneja wa NIHF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala na Mwimbaji wa nyimbo za Injili David Nyanda.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu akimkabidhi kadi ya uanacha wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mwimbaji nguli wa muziki wa Injili mzee Makasi mapema wikiendi hii wakati wa hafla ya uzinduzi wampango wa wanachama wa chama cha muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya. Katikati ni Meneja wa NIHF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala na Rais wa CHAMUITA Addo November.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala akielezea namna wanachama wanavyonufaiki na huduma za mfuko huo mapema wikiendi hii wakati wa hafla ya uzinduzi wampango wa wanachama wa chama cha muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) Addo November akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya KUTOKA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu akipokea risala ya Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) wakati wa uzinduzi wa kujiunga kwa wanachama wa chama hicho katika huduma ya Bima ya Afya kutoka kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Meneja wa NIHF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala, Mlezi wa chama hicho Askofu Dkt. Rejoyce Ndalima, Rais wa Chama hicho Addo November na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Bw. Makondeko.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu (wapili kushoto) akijumuika kucheza muziki wa injili mapema wikiendi hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na wana muziki wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) wakifuatilia zoezi la utoaji wa Ikadi za Bima ya Afya kwa wanachama wapya waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija

google+

linkedin