5/17/16

Watayarishaji wadogo wa muziki ni hatari sana – Mr T Touch


Mtayarishaji wa muziki Bongo Flava kutoka Free Nation, Mr T-touch amethibitisha kuwa watayarishaji wadogo wa muziki ni wabunifu na wajuzi zaidi.
t touch
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EATV, Mr T-touch alisema producers wadogo wanaupeleka muziki mbali.
“Unajua watu hawajui tu ila ukweli ni kwamba producers wadogo ni wazuri sana na wana uwezo mkubwa sema tu hawaaminiki sababu bado hawajatoboa na kuna dhana kuwa sisi yuliotoboa ndiyo wazuri lakini ukweli watarishaji wadogo wako vizuri kuliko hata sisi ambao tumetoboa kwenye muziki,” alisema Touch.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts