Watumishi hewa 11 watafuna Sh57.7 mil | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/13/16

Watumishi hewa 11 watafuna Sh57.7 mil

 
Halmashauri ya wilaya Nanyumbu imebaini watumishi 11 zaidi hewa ambao wamesababisha hasara kiasi ya Sh57,756,984.20 baada ya uhakiki.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbu, Idris Mtandi Katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbu kinachoendelea sasa.
Idris Mtandi amesema watumishi hewa wote wamebainika kuwa ni walimu wa shule za msingi na sekondari ambao wamekuwa wakipokea mishahara bila kufanya kazi.
Amesema changamoto kubwa ni namna taratibu za nidhamu zinavyotakiwa kuwa kwa kuwa mamlaka ya nidhamu ya walimu TSD  inavyochelewa kutoa maamuzi ya kinidhamu kwa walimu.
Hata hivyo, amesema mamlaka ya nidhamu ya walimu sasa itarudishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji ili aweze kuchukua hatua haraka kuliko ilivyo sasa

google+

linkedin