5/1/16

Wauza ‘Unga’ Watumia Shisha kunasa Vijana


SERIKALI imesema imebaini wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameanza kuchanganya tambaku ya shisha na dawa za kulevya aina ha Heroin na bangi ili kuvutia vijana kuanza kutumia dawa hizo.watumiaji wa shisha: picha-mitandao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2014.
Mhagama alisema kwa utafiti wa awali, serikali imebaini kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameamua kutumia mbinu hiyo ili kufanya vijana wawe watumiaji wa dawa hizo.
“Serikali imebaini mbinu mpya inayotumiwa na wafanyabiashara kuchochea matumizi ya dawa za kulevya nchini," alisema Mhagama na:
"Katika mbinu hiyo, tumbaku inayotumiwa kutengeneza Shisha huchanganywa na bangi au Heroin au vyote kwa pamoja, na kutumiwa bila watumiaji kujua jambo ambalo ni hatari.
“Utafiti wa kujua ukubwa wa tatizo unaendelea lakini hili tumeona tulisema kwanza kabla utafiti wenyewe haujaisha ili hatari zisiendelee kuwa kubwa.
"Serikali itaanza kwanza kupambana na wale wanaochanganya Shisha ambayo ni kiburudisho na dawa hizo za kulevya ili kuwavuta kuwa wateja wa dawa hizo.”
Mhagama alisema matumizi hayo ambayo yameonekana kushika kasi kwenye maeneo ya starehe, yamesababisha watumiaji wengi ambao ni vijana kuanza kutumia dawa hizo na kuwa wategemezi wake (mateja).
Katika hatua nyingine alisema kuwa, tani 15.7 zilikamatwa mwaka 2014, kiasi alichosema ni kikubwa kukamatwa nchini tangu mwaka 2009.
Alisema pia kuwa, katika mwaka huo kilo 400 za Heroin zilikamatwa kiasi alichosema ni kikubwa mara tatu kukamatwa tangu mwaka 2000.
Alisema katika mwaka huo, watuhumiwa 584 wa dawa za kulevya aina ya Heroin walikamatwa huku kilo 45 za Cocaine zikikamatwa na wafanyabiashara wake 351 wakikamatwa pia.
Alisema katika kutoa matibabu ya dawa za kulevya, mpaka Desemba 2014, kulikuwa na watumiaji wa heroine 1,787 wakiwamo wanawake 215 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya methadone, alisema.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts