5/3/16

Waziri Mwigulu awasilisha bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.


Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kuhusu mapitio ya utekelezaji kwa mwaka 2015/2016 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Magdalena Sakaya akiwasilisha Bajeti ya Kambi hiyo kuhusu mapitio ya utekelezaji kwa mwaka 2015/2016 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge akifafanua jambo wakati wa mjadala wa hoja ya makadirio ya matumizi ya wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 iliyowasilishwa Bungeni leo mjini Dodoma.   
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angellah Kairuki (wa kwanza kushoto mstari wa mbele) akifuatilia mjadala wa hoja ya makadirio ya matumizi ya wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 iliyowasilishwa Bungeni leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia mstari wa mbele ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju.
Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe leo Bungeni mjini Dodoma.
Wabunge wakifuatilia mjadala wa hoja ya makadirio ya matumizi ya wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 iliyowasilishwa Bungeni leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia mjadala wa hoja ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 iliyowasilishwa Bungeni leo mjini Dodoma.
Wanafunzi wa Kidato cha pili kutoka shule ya Sekondari Ihumwa iliyopo Manispaa ya Dodoma wakifuatilia mjadala wa hoja ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 iliyowasilishwa Bungeni leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo Anastasia Wambura akiteja jambo na Mbunge viti maalum kutoka mkoa wa Singida Martha Mlata  katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mpanda mjini Sebastian Simon Kapufi akifanya mahojiano leo mjini Dodoma na Mtandao wa Wanahabari Watoto kutoka jijini mwanza wakiongozwa na Mwanafunzi Getrude Clement (hayupo pichani) ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani. Wa kwanza kushoto ni mwanahabari kutoka Mtandao wa Wanahabari Watoto Happiness Christopher.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma alipotembelewa na Mwanafunzi Getrude Clement ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na  Mwanafunzi Getrude Clement alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, Dodoma)
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts