5/11/16

West Ham waitibulia Manchester United kuingia top 4


Klabu ya West Ham United imewaaga mashabiki wao vizuri katika uwanja wake wa nyumbani wa Upton Park kwa kutibua juhudi za Manchester United za kutaka kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne.
article-3583441-3405CF4D00000578-652_964x390
Ilikuwa mechi ya mwisho kuchezewa uwanja huo ambao umetumiwa na West Ham kwa miaka 112 kabla ya kuhamia uwanja wa Olimpiki.
Kwenye mechi hiyo ya kusisimua, West Ham walichomoza na ushindi wa 3-2.
3405ADFB00000578-3583441-image-a-128_1462915339418
Kuna vurugu zilitokea kabla ya mechi.
Man United ilikuwa inahitaji ushindi katika mechi hiyo na baadaye ushindi dhidi ya Bournemouth vingewahakikishia nafasi katika ligi kuu ya klabu Ulaya.
3405CCB200000578-3583441-image-a-137_1462918416071
Lakini kushindwa kwao kuna maana kwamba Manchester City, walio nambari nne, wamo alama nne mbele yao kabla yao kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Swansea City.
West Ham walitangulia kupitia bao la Diafra Sakho kipindi cha kwanza, lakini Antony Martial aliwasawazishia Red Devils kwa bao dakika ya 51 na kisha akawaweka kifua mbele dakika ya 72.
3405D03700000578-3583441-image-a-133_1462918401243
West Ham, hata hivyo, walijikwamua kwa kufunga mabao mawili ya kichwa katika kipindi cha dakika nne kupitia Michail Antonio na Winston Reid.
West Ham bado wana nafasi ya kumaliza katika nambari tano.
Wamo alama moja nyuma ya Manchester United na watazuru Stoke Jumapili.
Manchester United, watakuwa wenyeji wa Bournemouth, mechi ambayo watahitajika kushinda kujiimarishia uwezekano wa kumaliza katika nne bora.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts