5/11/16

Wizara ya Afya imewasilisha bajeti yake ya Bilioni 845


Mei 11 2016 Bunge la 11 limeendelea Dodoma, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017
Akisoma hotuba hiyo Waziri Ummy Mwalimu amesema…>>>’Hadi kufikia mwezi machi 2016 Wizara imekusanya jumla ya Shilingi 87,117,583,604 ikilinganishwa na makadirio ya Shilingi 122,998,941,500.00 yaliyoidhinishwa kwa mwaka 2015/2016
Hii ni asilimia 70.8 ya makadirio ya makusanyo ambayo yamevuka lengo kutokana na usimamizi thabiti na matumizi ya TEHEMA. Katika mwaka 2016/2017 Wizara inatarajia kukusanya Shilingi 163,755,679,857.00
Ili kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza kazi zilizopangwa katika mwaka 2016/2017, naliomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya makusanyo ya Shilingi 166,138,358,857 kutoka katika mashirika na Taasisi zilizopo chini ya Wizara yangu na vyanzo vya makao makuu
Aidha naomba Bunge likubali na kuidhinisha makadirio ya matumizi ya Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ya Shilingi 845,112,920,056.00 kati ya fedha hizo, Shilingi 317,752,653,00.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts