5/13/16

Youtube sasa kuanza kutumika kama app ya kutumiana ujumbe

YouTube inatengeneza mfumo wa kutuma ujumbe na kusambaza vitu kwenye mifumo ya simu ya Android na iOS katika jaribio la kuwabakiza watumiaji wake wanaotazama video hapo hapo.
YouTube-Gaming-AA-840x472
Tofauti na vitu vilivyopo sasa vya kuweka ujumbe na kusambaza, mfumo huo utakuwa zaidi wa kusambaza video ndani kwa ndani na kuchat na marafiki au kundi fulani. Tab mpya ya kushare itaonekana kwenye app ya simu itakayokuwa na video ulizoshare na mazungumzo na watu wako.
Utaweza kuandika ujumbe na kuweka emoji kama app zingine za kuchat na unaweza kulike comments, kuongeza marafiki kwenye kundi na kuangalia video zilizosambazwa na marafiki zako.
YouTube-sharing-menu-conversations-1
Huduma hiyo kwa sasa ipo kwa watu wachache tu.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm