Al-Shabab ladai kuwaua wapelelezi wa Kenya na US | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/11/16

Al-Shabab ladai kuwaua wapelelezi wa Kenya na US


wapiganajia wa kundi la Kigaidi la al-Shabab

Kundi la wanamgambo nchini Somalia, al-Shabab, wanasema wamewaua watu watatu kwa kuwapiga risasi na kumchinja shingo mwingine, baada ya kupatikana na hatia ya kuwa majasusi wa mashirika ya ujasusi ya Kenya na Marekani.

Mauaji hayo yalitekelezwa mbele ya umati wa watu katika mkoa wa Bakool.
Ahmed Godane

Kulingana na taarifa ya radio ya al-Shabaab, mwanamume mmoja aliyeuawa ni Mohamed Aden Nur, ambaye anashutumiwa kuwa aliwasaidia Wamarekani kumuua kiongozi wa kundi hilo Ahmed Godane.

Mwingine aliyepigwa risasi anadaiwa kuwa alisaidia Wamarekani kumuua Adnan Garaar, anayeaminika kuongoza shambulio la kigaidi katika duka la Westgate nchini Kenya mwaka wa 2013.

google+

linkedin