6/25/16

Algeria,Nigeria,Cameroon Na Zambia Kundi Moja Kuwania Kwenda Urusi 2018

World-Cup-2018-logo
Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF) mapema leo limetangaza makundi ya kuwania kwenda kwenye fainali za Kombe La Dunia mwaka 2018 zitakazofanyikia nchini Urusi.
Kutoka kwenye makundi haya, timu itakayoshinda na kuwa ya kwanza ndio itakwenda Urusi. Kwa maana hiyo Afrika itawakilishwa na timu 5 katika fainali za Urusi.
Michuano ya kuwania kwenda Urusi kwa upande wa Afrika itaanza mwezi October mwaka huu na kuendelea mpaka 2017.
Macho na masikio ya wapenzi wengi wa soka yameangukia kwenye Kundi B ambalo lina timu za Algeria, Cameroon, Nigeria na Zambia. Makundi yamepangwa hivi;
Kundi A: Tunisia, Libya, DR Congo, Guinea
Kundi B: Zambia, Cameroon, Algeria, Nigeria
Kundi C: Gabon, Mali, Ivory Coast, Morocco
Kundi D: Senegal, South Africa, Burkina Faso, Cape Verde
Kundi E: Ghana, Egypt, Congo, Uganda
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm