6/25/16

Aliyemuua Matonya Jela Miaka Mitano


MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu Baraka Hopaje (26) kwenda jela miaka mitano baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumuua Majuto Matonya bila kukusudia.
Pia, mahakama hiyo imeagiza mshtakiwa aendelee kupata huduma ya chakula maalumu pamoja na dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) kama alivyoandikiwa na daktari.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Ama- Isario Munisi.
Jaji alisema baada ya kupitia hoja zilizotolewa na pande zote mbili, ikiwemo maelezo ya onyo ya mshtakiwa aliyoyatoa wakati akihojiwa polisi pamoja na ombi lake la mazingira rafiki ya kutumia dawa na chakula pamoja na miaka minne aliyokaa mahabusu, smhtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu.
Pia, mahakama imesikiliza hoja za Jamhuri kwamba mshtakiwa amefupisha maisha ya Matonya na kwamba amekufa na kuacha familia iliyokuwa ikimtegemea hivyo mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho.
Akifafanua alisema pamoja matumizi ya dawa hizo kwa watu wanaovunja sheria isiwe kigezo cha kushindwa kuwajibishwa kama sheria inavyoelekeza na kwamba bila kuwapa adhabu zinazostahili matukio yataongezeka mara dufu kwa kivuli cha sababu hiyo.
Jaji alisema kwa sababu mshtakiwa alitoa ushirikiano alipohojiwa na polisi lakini kitendo cha kukatisha uhai wa Matonya hakiungwi mkono pamoja na kukaa mahabusu miaka minne atakwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitano
Mapema juzi, mshtakiwa huyo alikiri kumuua Matonya bila kukusudia kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi.
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Agosti 12, mwaka 2011 katika baa ya Mashujaa mshtakiwa akiwa kazini kama kaunta wa baa hiyo alimuua bila kukusudia Matonya baada ya kutokewa ugomvi uliosabishwa na wivu wa mapenzi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts