6/20/16

Apigwa risasi akiwa ‘live’ Facebook


Mtu mmoja Chicago, Marekani amepoteza maisha kwa kupigwa risasi ya kichwani wakati akiwa ‘live’ katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Mtu huyo ambaye anafahamika kwa jina la Antonio Perkins, 28 alikuwa live na marafiki zake lakini ghafla kulisikika mlio wa risasi ambapo baadae Polisi Chicago walitoa taarifa ya mtu huyo kuuwawa.

Video ya mtu huyo wakati akiwa live bado ipo katika mtandao wa Facebook na mpaka sasa zaidi ya watu 700,000 wameshaitizama video hiyo.

Aidha taarifa zinaeleza kuwa mpaka sasa hakuna mtu ambae amekamatwa kutokana na tukio hilo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts