6/21/16

Ashtakiwa kwa kumtusi rais Magufuli mtandaoni
Raia mmoja wa tanzania anakabiliwa na mashataka baada ya kusambaza maoni yake ya mtandao wa WhatsApp akimuita rais john Pombe magufuli mpumbavu.

Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria uhalifu wa mtandaoni.

Ni mtu wa pii kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa kumtusi rais.

Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanzishwa mwaka uliopta.

Hivi ndivyo alivyoandika:''Kwani rais Magufuli hana washauri?haushauriki? Ama ni mjinga tu?Ni Mpumbavu sana;Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?

Jina Mnyika lililotajwa ni la Mbunge John Mnyika nchini humo ambaye anajulikana kwa kuzungumza sana.
 Chanzo: BBC
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts