6/13/16

Askari wasiowapigia saluti wabunge kukatwa mishahara

 Askari akimpigia saluti mbunge wa Arumeru
Serikali imetangaza adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine askari polisi wote nchini ambao hawatawapigia saluti wabunge wa Bunge la Muungano  na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Agizo hilo limetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Umwagiliaji William Ole Nasha wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Ole Nasha amesema kumpigia saluti mbunge ni jambo la lazima kwa askari kwa kuwa lipo kwenye moja ya masharti yao, hivyo kutokufanya hivyo ni kushindwa kutii kiapo cha uaminifu wao.
Ole Nasha  alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Fakharia Shomar Khamis (CCM) ambaye alitaka kujua ni adhabu kiasi gani atapewa askari ikiwa atashindwa kutoa saluti kwa mbunge.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm