6/18/16

Auawa akiwakimbia polisi

Mtu anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akifanya jaribio la kuwatoroka polisi waliomkamata akiwa na silaha ya kivita aina ya AK 47 aliyoficha kwenye mfuko wa kuwekea kompyuta mpakato.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amemtaja aliyekamatwa na silaha hiyo kuwa alitambulika kwa jina la Benjamin Wales (Singano).
Amesema alikamatwa jana saa 11.30 jioni katika kizuizi cha  polisi kilichopo Chekelei, Wilaya ya Korogwe katika barabara kuu ya Segera - Njiapanda ya Himo akisafiri na basi la kampuni ya Lakome likitokea Karatu kwenda Dar es salaam.
Kamanda Paulo alisema baada ya askari kulisimamisha basi hilo na kufanya upekuzi walibaini kwenye mfuko wa Benjamin umewekwa nguo pamoja na silaha aina ya AK 47, magazine mbili na risasi 37 vyote vikiwa vimefungwa na karatasi la nailoni.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts