6/9/16

Bajeti 2016/17: Wasanii, Wabunifu na Wanamichezo watengewa bilioni 3

Serikali itatenga kiasi cha shilingi bilioni tatu kwaajili ya kusaidia kazi za wasanii, wabunifu na wanamichezo.Kiasi hicho cha fedha kimependekezwa kwenye makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 kama yalivyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.

“Katika mwaka 2016/17 serikali kupitia fungu 96 imetenga jumla ya shilingi bilioni 3.0 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya sanaa, ubunifu, utamaduni na michezo ikiwa ni pamoja na: kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Ubunifu; kusimamia urasimishaji wa shughuli za Sanaa; kusimamia na kudhibiti filamu zitakazoingia sokoni bila kufuata taratibu; na kuratibu uendeshaji wa kazi za sanaa nchini,” imesema hotuba ya Dkt Mpango.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts