6/19/16

Bashe aja na marekebisho kibao ya Bajeti
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amejiandaa kumbana Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kwa kupeleka jedwari la marekebisho la kuondoa ongezeko la kodi katika magari, bodaboda na mitumba katika Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha.


Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma jana, Bashe alisema atapeleka marekebisho hayo leo.


Alisema marekebisho mengine ni kodi katika utalii, kufuta kodi katika mazao yasiyosindikwa, uhamishaji wa fedha na Sheria ya Mawasiliano ambayo inalazimisha kampuni za simu kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).


Alipinga kulazimisha makampuni ya simu kujisajili katika soko hilo ndani ya miezi sita kwa sababu hiyo itaua thamani za kampuni hizo.Alisema badala yake serikali iweke vivutio kama kupunguza kodi mbalimbali, hali itakayofanya kampuni si tu ya simu bali na mengine
kujiunga na soko hilo.
“Pia nimeishauri vyanzo vingine vya mapato ambavyo havitaathiri bajeti kuu. Wao kama ni mabadiliko ya sheria kuwezesha vyanzo vipya ninavyovishauri wavilete kwenye Bunge la mwezi wa tisa,” alisema.
Alivitaja vyanzo vipya vya mapato ni pamoja na uvuvi katika bahari kuu ambapo kutakuwa na mapato ya Sh200 bilioni.
“Kwa kuanzisha soko la madini, watu wawe wanaingia na madini yao bila kutozwa ushuru tutapata fedha kwa kulala katika hoteli, kununua vitu na tutakayotoza kwa kuuza madini nje ya nchi,” alisema.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts