6/27/16

Billnass ndiye mwanzilishi wa label ya ‘LFLG’, ni ile inayomsimamia Nuh pamoja na yeye mwenyewe

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Billnass amefunguka kwa kusema kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa label ya ‘LFLG’ ambayo pia inamsimamia Nuh Mziwanda.
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’, mwanzoni mwa mwaka huu alitangaza kuachana na label ya Rada Entertainment ya TID na kujiunga na ‘LFLG’ ambayo amedai ni yake.
Akiongea katika kipindi cha Global TV, Billnass aliulizwa kama ni kweli amesainiwa ndani ya label hiyo pamoja na Nuh Mziwanda.
“Management yangu mpya ya ‘LFLG’ mimi ndiye founder wa hiyo ‘LFLG’,” alisema Billnass. “Hii nilianza nayo nikiwa na Mchafu tukalileta wazo kibiashara zaidi. Kwa hiyo mimi nipo nao toka inaanza, Nuh Mziwanda ndo amekuwa signed hivi karibuni lakini mimi nipo nao toka naanza, yaani toka nikiwa Rada nilikuwa na mawazo ya kuanzisha kitu kama hicho,”
Rapper huyo ambaye mpaka ana ngoma 4, anafanya poa katika vituo mbalimbali vya radio kutoka na kutoa ngoma kali ambazo zinakubalika na mashabiki.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts