6/2/16

Bomoboamoa yatikisa mjini Bukoba
Manispaa ya Bukoba imebomoa vibanda na kuwaondoa wafanyabiashara wadogo mitaani, chini ya ulinzi wa polisi na mgambo wenye silaha.


Kutokana na hatua hiyo kuchukuliwa chini ya ulinzi wa polisi, wafanyabiashara hao hawakuonyesha ukaidi badala yake walikuwa wanahangaika kuhamishia bidhaa zao.


Bomoabomoa hiyo imewakumba wafanyabiashara waliokuwa nje ya lango la hospitali ya Rufani Mkoa wa Kagera, eneo ambalo lilikuwa na wamachinga wengi zaidi ikilinganishwa na mengine ya mji wa Bukoba.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Wallace Karia amesema zoezi hilo halikupata vikwazo kwa sababu walikubaliana nao kuwa, wangehama Februari kwenda eneo walilopangiwa.
 
chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts