6/9/16

Bongo kupata location ni ngumu sana – Msafiri (Kwetu Studios)


Muongozaji wa video za Bongo ambaye anafanya vizuri Msafiri Shabani kutoka kampuni ya Kwetu Studio amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo waongozaji wa hapa nchini ni location.

Akiongea na E-Newz ya EATV, Msafiri alisema ameanza kwenda kufanya video zake Afrika Kusini kutokana na uhakika na uharaka wa upatikanaji wa vitu kwaajili ya kazi zao kwakuwa kwa Tanzania inachukua muda mrefu wa kupata ruhusa ya kukamilisha kazi zao. 
 “Unakuta unaambiwa uandike barua, barua yenyewe inaweza ikaenda kujadiliwa mpaka wewe unakuja kupewa jibu tayari umeshaenda South Afrika umeshuti na tayari video umeshatoa. Hata katika location unakuta mtu mpaka akugeie gari ama nyumba mpaka muwe mnajuana wakati ukienda South chochote unachokitaka vipo vya kukodi ni wewe tu ukiwa na pesa,” alisema.
Pia Msafiri aliongezea kuwa sababu nyingine inayowafanya wakashuti video hizo nje ni kutokana na kuangalia wengine wanafanya nini ili nao waweze kushika nafasi nzuri katika soko la ushindani pia akidai kuwa inasaidia kupandisha thamani ya msanii kwakuwa anaonekana ana uwezo wa kutengeneza pesa kwaajili ya kufanya kazi zake.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts