6/10/16

Chadema wakomaa na mikutanoMwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.
By Peter Saramba, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mwanza. Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, wamekitaka chama hicho kuendelea na ratiba yake ya mikutano ya hadhara bila kujali zuio la Polisi kwani halina misingi ya kisheria.

Viongozi wa Chadema, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji jana walijifungia kutwa nzima Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza kujadili hatua za kuchukua dhidi ya kitendo cha Polisi kuzuia maandamano na mikutano ya chama hicho.

“Tutatoa kauli rasmi kesho (leo), baada ya vikao. Ninachoweza kuthibitisha ni kwamba tunaendelea kushauriana njia sahihi ya kuchukua,” alisema Mbowe.

Baadhi ya mawakili wa Chadema akiwamo Paul Kipeja na John Mallya, jana walionekana katika viunga vya hoteli hiyo katika kilichoelezwa na vyanzo vyetu kuwa ni maandalizi ya chama hicho kufungua shauri mahakamani dhidi ya Polisi.

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitiawww.epaper.mcl.co.tz
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts