6/19/16

CRDB yatoa madawati 60 Muheza

 

Picha ya Maktaba.
Benki ya CRDB imetoa madawati 60 yenye thamani ya Sh5 milioni kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli kupambana na uhaba uliopo kwenye shule mbalimbali hapa nchini.
Meneja wa CRDB Mkoa wa Tanga, Evarist Mnyele  amemkabidhi rasmi madawati hayo Mkuu wa wilaya ya Muheza, Esteria Sekilasi.
Akizungumza wakati wa  makabidhiano hayo, Mnyele amesema wameamua kutoa msaada huo ili kurudisha faida kwa wananchi kwa sababu benki hiyo imetokana nao, hivyo kuna kila sababu ya kusaidia shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza baada ya kupokea madawati hayo, Kilasi aliishukuru benki hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia kupunguza uhaba wa madawati wilayani humo na kwamba yatasambazwa katika shule mbalimbali.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts