6/21/16

CUF Mwanza yamtaka Lipumba asubiri uchaguzi

CHAMA cha Wananchi (CUF), mkoani hapa kimewaambia wanachama wa chama hicho kuwa, aliyekuwa Mwenyekiti wao Prof. Ibrahimu Lipumba, hawezi kuruhusiwa kuendelea na wadhifa wake kama alivyoomba, badala yake asubiri uchaguzi mkuu ili aombe kuwania tena.

Akizungumza na Nipashe katika ofisi za wilaya za chama hicho jana, Katibu wa Wilaya wa CUF, Rehema Mwendwa, alisema Prof. Lipumba, hakuondoka katika chama kwa ugomvi bali kwa sababu za kupinga maamuzi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumsimamisha, Edward Lowassa, kuwania nafasi ya Rais kwa tiketi ya umoja huo.
"Kutokana na maamuzi yake hayo, Prof. Lipumba, hakuvuliwa uanachama bali ni maamuzi yake binafsi, hivyo yupo wazi kuchukua tena fomu na kuwania nafasi hiyo kipindi kijacho, lakini si kwa kurejea kwa kuikana barua yake ya kujizulu,” alisema.
Alisema Lipumba ana haki ya kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi kutokana na mamlaka yakitokea kwenye mkutano mkuu, kwa sasa chama kina nafasi sita za wazi zikiwamo za mwenyekiti na makamu wake na hao watapatikana katika uchaguzi wa Agosti 21, mwaka huu.
Naye mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo, Salumu Mkumbukwa, alimtaka Rais John Magufuli, kutoa tamko kuhusu polisi kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa hali inayoiondoa nchi kwenye nchi ambazo hazina demokrasia.
"CUF wilayani Nyamagana, tunamuomba Rais Magufuli aruhusu mikutano ya vyama vya kisiasa, kwani kuvibana kutaifanya nchi kukosa demokrasia kwani vingi vinajipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao baada ya kuona makosa waliyofanya,” alisema.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm