6/21/16

Familia moja Magomeni DSM yazua Kizazaa
Familia moja ya jijini Dar es salaam imezua kizazaa nyumbani kwa David Mwamkinga anadayeiwa kuwa ni mchungaji wa kanisa ambalo halijulikani jina baada ya kuamua kumtoa kwa nguvu ndugu yao aliyefahamika kwa jina la Bakari Mwaisumo ambaye anadaiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo zaidi ya miezi mitano bila kutoa taarifa kwa ndugu zake.

Ndugu hao wamefika nyumbani kwa Bwana Mwamkinga eneo la Magomeni Kagera na kumkuta ndugu yao amekaa nje ya nyumba (uwani) akijisomea kitabu ambapo walimuomba arudi nyumbani na dakika chache baadae alitokea Bwana Mwamkinga ambaye aliulizwa sababu za kuishi na bwana Mwaisumo wakati ana nyumba yake jirani tu na hali ilikuwa hivi.

Baada ya mvutano na majadiliano ya muda mrefu ndugu hao walimlazimisha bwana Mwaisumo kurudi nyumbani kwake huku wakimshurutisha mchungaji Mwamkinga kuwapa kadi ya gari, hati ya nyumba na nyaraka ambazo wamedai kuwa ndugu yao aliondoka nazo pindi alipohamia kwenye nyumba hiyo. Hatimaye Bwana Mwaisumo alikubali kuondoka na ndipo ndugu zake walipokusanya nguo na vitu vyake na kuvihamishia nyumbani kwake.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm