First Lady Michelle Obama Ajiunga Na Snapchat | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/22/16

First Lady Michelle Obama Ajiunga Na SnapchatFirst Lady Michelle Obama

Hakuna shaka kwamba Michelle Obama akiondoka Ikulu ya Marekani (White House) hapo Januari mwakani ataacha historia ya kuwa one of the coolest First Ladies the USA ever. Hakuna ambacho hajakifanya mpaka sasa. Haishangazi kwamba ana ushawishi mkubwa sana sio tu miongoni mwa wasichana bali wanawake na wanaume kwa ujumla.

Katika kuongeza “cool factor” amejiunga na mtandao wa kijamii unaokua kwa kasi wa Snapchat. Anatumia jina la michelleobama . Kwa wale ambao mna makazi kwenye snapchat mnaweza kumfuata First Lady ambaye amesema kupitia mtandao huo atakuwa akiweka kila kitu atakapokuwa safarini wiki ijayo nchini Morocco,Spain na Liberia. Huko anatarajiwa kuonana na wasichana wasioenda shule katika mojawapo ya kampeni zake kusisitiza kuhusu elimu hususani kwa watoto wa kike.

Michelle Obama tayari ana followers kama milioni 4.5 kwenye Twitter na milioni 5 kwenye Instagram.

google+

linkedin