6/2/16

Fisi Wafukua Makaburi Shinyanga
Huduma muhimu za maabara Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), zimesimama baada ya vipimo vya damu, ini na figo kuharibika na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa.


Mamia ya wagonjwa ambao walihitaji huduma hiyo, waliondoka hospitalini hapo bila kuhudumiwa kutokana na ubovu wa vifaa hivyo.


Mmoja wa wagonjwa waliopatwa na mkasa huo, Simon Japhet aliliambia Mwananchi kuwa alifika hospitalini hapo na kuchukuliwa kipimo cha damu Jumatatu, lakini mpaka Jumatano hakuwa amepatiwa majibu.


Mhudumu wa maabara hospitalini hapo ambaye hakutaka kutajwa, alisema vipimo hivyo viliharibika kwa nyakati tofauti na kwamba hakuna matengenezo yaliyofanyika.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts