6/28/16

Hakimu, wakili waonyeshana umahiri wa sheria
Mabishano ya kisheria yameibuka katika Mahakama ya Mkoa wa Wete, kati ya hakimu na wakili wa utetezi kuhusiana na tuhuma zinazowakabili watuhumiwa watano.


Watuhumiwa hao wanadaiwa kuharibu mali kwa kukata mikarafuu minne, minazi mitano na mashina ya mihogo wiki iliyopita, mali ya Ali Khamis Othman.


Kabla ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Khamis Smai ambaye alitarajiwa kuisikiliza alisema kwa mujibu wa sheria na taratibu, inapaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo.


Wakili wa upande wa utetezi, Suleiman Khalfan alipinga shauri hilo kuhamishiwa Mahakama ya Mwanzo hivyo kuzusha mabishano yaliyochukua takriban dakika 30.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts