6/10/16

Ilala yaanza kumsaka chatu wa Mto Mzinga
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imedhamiria kumsaka nyoka aina ya chatu anayeishi karibu na Mto Mzinga ambaye amekuwa tishio kwa wakazi wa eneo la Lubakaya, Kata ya Zingiziwa.
Nyoka huyo amekuwa akionekana kati ya saa 12 hadi saa 1 jioni akitokea kwenye mto huo na kuelekea kwenye makazi ya watu kula mifugo, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Isaya Mngurumi amesema chatu huyo alionekana mara moja, hivyo ofisi hiyo imetuma wataalamu ambao watashirikiana na diwani wa kata hiyo kumsaka

Mngurumi alisema mwanzo alituma watu kutoka kwenye halmashauri hiyo ambao walishirikiana na wananchi wa eneo hilo kumsaka chatu huyo lakini hawakufanikiwa.
“ Mwanzo niliagiza timu yangu ambayo walishirikiana na wananchi akiwemo diwani wa eneo hilo, lakini hawakumpata hivyo nimeamua kutuma wataalamu waweze kumsaka chatu huyo,” amesema.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm