6/1/16

Jay Moe kuvunja ukimya wa miaka 4 kwenye muziki kwa kuachia wimbo ‘Pesa ya Madafu’

Jaymoe
Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Jay Moe amesema ukimya wake wa muda mrefu umemfanya ajiandae vizuri ili asiwaangushe mashabiki wake.
“Nina project mpya ya Jay Moe mwingine, baada ya miaka 4 toka 2012 ndio last time nilifanya muziki,” alisema Jay Moe. “Kwa hiyo imenichukua miaka 4 ya kuweza kujipanga tena, na kusema kwamba sasa hivi nikirudi, watu watasema safi, kitu tulichokuwa tunakisubiria tumekiona kwa sababu itakuwa ni aibu baada ya miaka yote 4, alafu nakuja nawaangusha watu,”
Aliongeza, “Project yangu mpya, inaitwa Pesa ya Madafu, ni wimbo ambao nimefanya mwenyewe chini ya producer chipukizi, Daz Knowledge. Pia wiki hii mungu akipenda tutaachia na video yake, itakuwa ni miaka 11 toka Jay Moe mara ya mwisho aachie muziki video ya wimbo,”
Jay Moe ni mmoja kati ya marappa wachache wa bongo ambao walifanya vizuri kipindi cha nyuma na kujizolea mashabiki wengi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts