6/20/16

Kahama kupata neema ya umeme

 
Wakazi wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga wanatarajia kupata umeme kutoka mgodi wa Buzwagi.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kahama, Sule Kabati amesema hayo alipokuwa akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya hiyo, Vita Kawawa aliyetembelea mradi wa mtambo wa kuunganisha umeme kutoka katika mgodi huo.
Meneja huyo alisema kuunganishwa na kuwashwa kwa mtambo huo kutamaliza tatizo la kukatika umeme uliokuwa ukiukabili mji huo na vitongoji vyake.
 “Pia, mtambo huu utaongeza uwezo wa Tanesco wa kuhudumia wateja wengi zaidi kulinganisha na awali,” amesema Kabati.
Umeme huo unatarajiwa kuwashwa Juni 24, mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm