6/30/16

Kidiaba ampeleka Ajibu sokoni

 
Dar es Salaam. Kipa wa TP Mazembe, Robert Muteba Kidiaba amefichua siri kuhusu uongozi wa timu hiyo unamfuatilia mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu.
Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe, Kidiaba alisema klabu yao ina taarifa zote kuhusu Ajibu na inaendelea kufuatilia maendeleo ya mchezaji huyo.
“Labda nikwambie tunawafuatilia wachezaji wa Simba, hasa baada ya kumnunua Samatta, ambaye alifanya vizuri, kuna kijana anaitwa Ajibu (Ibrahim), huyu taarifa zake tunazo, kikubwa aendelee kufanya vizuri.
“Uongozi wa timu uliridhishwa na uwezo wa Samatta na ndiyo maana Tanzania ni sehemu ambayo Mazembe inasaka vijana watakaoisadia huko mbeleni,” alisema.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts