6/19/16

KIKWETE :Serikali pekee haiwezi kutatua changamoto za elimu

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amesema licha ya kwamba upatikanaji wa elimu ya msingi na sekondari ni bure, Serikali pekee haiwezi kutatua changamoto zilizopo.
Kikwete amesema hayo jana wakati wa matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia gharama za elimu yanayoendeshwa na Taasisi ya Binti Foundation kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Kikwete, ambaye aliongoza Serikali ya Awamu ya Nne amesema mtoto anayeishi katika mazingira ya umaskini, elimu bure bado inakuwa ni changamoto kwake kwa ana mahitaji mengi ambayo mzazi anatakiwa ayagharamie ikiwamo chakula, sare za shule na mengine muhimu.
“Mtoto anayehudhuria masomo lakini nguo zake zimechanika, atakuwa darasani, hana furaha atabaki mnyonge tofauti na wenzake. Hapo atashindwa kuitumia ipasavyo haki yake ya msingi ya kupata elimu kutokana na mazingira anayoishi,” amesema Kikwete.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm