Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

6/20/16

Kwa ukali wa ‘Jike Shupa’ ni muda wa kuanza kumchukulia ‘serious’ Nuh Mziwanda

Kuna ngoma mpya mbili tatu za Bongo Flava ambazo kila nikizisikia au nikiziona nikiwa busy kwenye computer kufanya kazi yangu ya kila siku (kuandika makala na habari), hujikuta nikisimama kidogo kuzipa ‘attention’ inayostahili. Ni kwasababu ya utamu wake au tu kwa jinsi video zake zilivyo nzuri.
image
Kutaja chache tu, baadhi ya nyimbo hizi ni pamoja na Ibaki Story ya Rich Mavoko na Jike Shupa ya Nuh Mziwanda aliyomshirikisha Alikiba. Nafahamu kuwa ni Ibaki Story ya Mavoko ndiyo iliyotrend zaidi kutokana na kuambatana na ile habari kubwa ya mkali huyo kujiunga na WCB. Jike Shupa iliyoanza kutoka ilitrend kwa kiasi chake na hasa kwakuwa Alikiba alishirikishwa na kama unavyojua ana fan base kubwa, lakini sidhani kama watanzania wanajua ukubwa wa wimbo huu.
Niseme tu kuwa thamani ya wimbo huu imeongezeka zaidi baada ya video yake kutoka. Na kiukweli nampa tano muongozaji, Msafiri kwa si tu kutoa video safi, bali kwa story nzima iliyobeba ujumbe wa wimbo huo. Tangu wimbo ulipotoka, wengi tuliamini kuwa Nuh alimuimbia ex wake Shilole. Hiyo ilipelekea hadi watu wakaanza kumuita Shishi jina hilo. Ubashiri huo ulikuja kuonekana ni wa kweli baada ya video yake kutoka.
Kwenye video hiyo ametumika msichana anayefanana na Shilole kama pacha wake. Kama ilivyotegemewa, video hiyo haijayapendeza macho ya Shishi na hivyo kupelekea vita vya maneno kati yao kwenye mitandao ya kijamii.
Tuachane na vita hiyo kwanza bali nataka nikueleze kwanini ni muda sasa wa kuanza kumchukulia serious Nuh kama muimbaji mwenye kipaji. Mwaka 2014 nilimweka kwenye orodha ya wasanii wa kuwaangalia baada tu ya kuona wimbo wake wa kwanza, Otea Nani. Sina uhakika kama huu ndio ulikuwa wimbo wa kwanza bali mimi nilimfahamu kupitia wimbo huu.
Baada ya hapo alitoa ngoma kadhaa zikiwemo Zima Taa, Msondo Ngoma, Bilima, Ganda la Ndizi na Hadithi. Lakini hadi sasa Jike Shupa ndiyo umekuwa wimbo mkubwa zaidi katika career yake. Na hiyo haijatokana na kumshirikisha Kiba pekee, bali ngoma hii ni kali. Chorus ya Alikiba ni tamu na imeimbwa kiufundi huku ukijikuta ukiwa na hamu ya kuisikia mara nyingi. Ni wimbo mkubwa na kwa sikio la mtu asiye na ushabiki, ni dhahiri atakuwa ameongeza heshima kwa Nuh na kuanza kumchukulia serious.
Ni kwamba watu waliacha kumchukulia maanani Nuh kipindi yupo kwenye uhusiano na Shilole. Jina lake lilikuwa kubwa sana lakini si kwasababu ya nyimbo zake, bali kwasababu alikuwa boyfriend wake na Shilole. Alikuwa hakosekani kwenye headlines si kwasababu ametoa wimbo mkubwa au kapiga bonge la show sehemu, bali ni kwasababu imesemekana amepigwa vibao na mpenzi wake, amepost picha akioga bafuni na Shishi au wamedaiwa kuachana! Nuh alikuwa maarufu kutokana na ‘controversy’ zilizokuwa zimeizunguka couple yao.
Kwahiyo watu waliacha kumchukulia Nuh kama msanii, bali kama ‘serengeti boy’ aliyekuwa amezama kwenye penzi na supastaa.. Kwa lugha nyingine, Nuh alipata jina, lakini kimuziki alishuka. Yeye pia alikiri hilo kwa kudai kuwa uhusiano na staa huyo ulimpoteza. Hii ilikuwa natural kabisa na wala simnyooshei kidole Shishi kuwa hakuwa girlfriend sahihi kwa kijana huyu, bali aina ya maisha yao ilipelekea tu Nuh kupotea kwenye ramani ya muziki na kuwa maarufu kwenye ramani ya skendo.
Na kama unavyojua promota hamuiti msanii kwasababu ya skendo zake, bali humuita kwasababu ya hits zake. Kwa mazingira hayo Nuh alikuwa supastaa kutokana na skendo lakini watu walianza kumsahau kuwa ‘the boy can actually sing and has pure talent.’
Na nina uhakika kuna watu wengi sana walikuwa hawajui hata nyimbo zake lakini walimjua kutokana na skendo za uhusiano wake wa zamani. Nimekutana na Nuh kwa mara nyingi na kiukweli anajielewa sana. He is actually very smart!
Kwahiyo ni muda sahihi sasa watu wakaanza kumchukulia serious kijana huyu kuwa ana uwezo mkubwa katika uimbaji. Jike Shupa imedhihirisha uwezo wake na hakuna anayeweza kubisha kuwa ni wimbo unaochezwa sana kwa sasa.
Na kwa Nuh anachotakiwa kufanya sasa ni kuwaonesha watanzania kuwa anaweza na kwamba si mtu anayetegemea mwanamke ampe kiki. Ni muda sasa wa kumpa sikio jamaa huyu kusikiliza muziki wake na kumpa heshima anayostahili.