Lwenge atangazia vita watendaji wabovu wa mamlaka za maji | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/10/16

Lwenge atangazia vita watendaji wabovu wa mamlaka za maji


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge amesema mtumishi yeyote wa mamlaka ya maji nchini atakayebainika kuihujumu mamlaka atafukuzwa na nafasi yake itatangazwa upya.


Lwenge ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Dodoma (Duwasa).


Amesema ili mamlaka za maji nchini zisonge mbele, zinahitaji watumishi wenye maadili.


“Tukipata habari wote tutawaondoa…. fanya kazi kulingana na maadili ya kazi lakini sio mnahujumu mamlaka na mwisho wa siku mnagawana fedha pembeni,” Amesema Lwenge.

google+

linkedin