Mahafali yamzuia Obama kumzika Muhammad Ali | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

6/9/16

Mahafali yamzuia Obama kumzika Muhammad Ali

 

Rais wa Marekani,Barack Obama .
Louisville, Marekani. Ikulu ya Marekani imesema Rais Barack Obama na mkewe, Michelle watakuwa shuleni katika mahafari ya mtoto wao, Malia, hivyo hawatahudhuria maziko ya nguli wa masumbwi duniani, Muhammad Ali.
Badala yake, watatuma barua kwa familia ya Ali kupitia kwa Mshauri Mkuu wa Ikulu, Valerie Jarrett, ambaye anamjua Ali.
Mazishi hayo yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa mjini Louisville, Kentucky, ambako Ali alizaliwa, yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais mstaafu wa Marekani, Bill Clinton.
 Bob Gunnell, Msemaji wa familia ya Ali, alisema Obama na mjane wa Ali, Lonnie walizungumza kwa njia ya simu.

google+

linkedin