6/30/16

Mahakama ya mafisadi kuanza rasmi Julai mosi 2016
Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameahirisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi kujiuliza mara mbili kabla ya kufanya uharifu baada ya mahakama ya mafisadi nchini kuanza kazi rasmi Julai mosi 2016.
Akizungumza wakati wa kuahirisha mkutano huo, Mhe Majaliwa amesema kufuatia kuanzishwa mhakama hiyo sasa serikali inafanya marebisho ya sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 ili kuongeza ukubwa wa adhabu zitakazolewa na hivi sasa na mahakama hiyo.

Akizungumzia hatua ya kambi ya upinzani kutohudhuria vikao vya bunge Mhe. Majaliwa amesema kumekuwa na taswira potofu inayojaribiwa kujengwa ili kuonyesha kunakuminywa kwa demokrasia bungeni, na kusisitiza wahisani wamebaini upinzani nchini bado hauja komaa kisiasa kwa kuwa kutoingia bungeni kunaweza kusiwe na tija kwa wananchi wanaowawakilisha.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amepongeza wananchi waliojitokeza kuchangia madawati na kusisitiza mbaka sasa madawati mapya laki 5.52 yamepatikana kwa njia ya michango hatua iliyofanya shule za msingi kuwa na madawati zaidi ya milioni 2.6 sawa na asilimia 77 ya mahitaji hivyo bado kuna upungufu wa madawati laki 7.9

Akiwasilisha taarifa ya Spika, sakata la kampuni ya Lugumi, Naibu Spika Mhe Tulia Ackson amesema kwa mujibu wa kanunu ya 17 fasiri ya 17 imeitaka serikali kuhakikisha mfumo wa utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya polisi ifanye kazi ndani ya miezi mitatu kutoka sasa.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts