6/21/16

Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu yakabidhi madawati 1380 Shinyanga

Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga imekamilisha zoezi la kutengeneza madawati kwa shule zake za msingi na sekondari kufuatia Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kukabidhi jumla ya madawati 1380 huku mkuu wa wilaya hiyo, Vita Kawawa akiagiza zoezi endelevu la utengenezaji madawati kuwa Ajenda ya Kudumu ya halmashauri hiyo.

Makabidhiano ya Madawati hayo yamefanyika katika ofisi za halmashauri ya Msalala, kati ya mwekezaji huyo mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA na Mkuu huyo wa wilaya ikiwa ni madawati 1080 kwa shule za msingi na 300 kwa shule za sekondari hivyo kukamilisha upungufu wa madawati yaliyokuwa yanahitajika.

Kukamilika kwa zoezi hilo la madawati sasa kazi ni moja kwa maofisa elimu ni kuhakikisha wanaboresha kiwango cha taaluma kinachotolewa kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm