6/21/16

Mhariri Dira ya Mtanzania kizimbani kwa Kuchapisha habari "Kifaru cha Kivita cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), kimeibiwa’

Mhariri wa Gazeti la wiki la Dira ya Mtanzania, Musa Mkama amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kusababisha hofu kwa jamii.


Mbali na Mkama, pia mwandishi wa gazeti hilo Prince Newton naye alipandishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Respicius Mwijage.


Akisoma hati ya mashtaka jana, Wakili wa Serikali Mkuu, Timoth Vitalis akisaidiana na wakili Hellen Moshi alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Juni 20, mwaka huu katika eneo la Biafra lililopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Ilidaiwa kuwa kuwa siku ya tukio katika eneo hilo, washtakiwa hao kwa pamoja walichapisha taarifa ya uongo katika gazeti la Dira ya Mtanzania toleo namba 424 la tarehe 20/6/2016 lenye kichwa cha habari ‘Kifaru cha Kivita cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), kimeibiwa’.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm