6/2/16

Misaada kutoka Ulaya haikwepeki – Kikwete

Rais mstaafu wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika lazima zijiwekee utaratibu wa namna ya kupokea misaada  kutoka nchi za Ulaya, kwa kufuata sheria za nchi husika na zile za kimataifa.
Kikwete  alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili malengo mapya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayohusu ‘Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2030’.
Alisema nchi hizo haziwezi kukwepa misaada kutoka nchi za Ulaya kwa kuwa misaada hiyo ni jukumu lao la kihistoria.
Alisema jukumu hilo linapaswa kuendelezwa kwa kuwa maendeleo ya nchi za Ulaya yalitokana na rasilimali walizozitoa Afrika kipindi cha ukoloni.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Kikwete imekuja wakati Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli amekwisha kuweka msimamo katika hotuba zake kadhaa akitaka Tanzania ijitegemee kwa asilimia kubwa badala ya kutegemea misaada ya nje.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts