6/27/16

Mkuu wa mkoa Dsm Paul Makonda amemsimamisha kazi Msimamizi mkuu wa barabara
Mkuu wa mkoa Dsm Paul Makonda amemsimamisha kazi Msimamizi mkuu wa barabara katika mkoa wa dsm Injinia Josephat Shehemba kutokana na barabara nyingi katika jiji la dsm kujengwa chini ya viwango,kushindwa kusimamia wakaguzi wa ubora wa viwango na kushindwa kutimiza wajibu wake kikazi.

Sambasamba na kusimamishwa huko Vyombo vya Uchunguzi ikiwemo takukuru wamepewa jukumu la kumchunguza pamoja na kuchunguza makampuni ya Ukandarasi yaliyopewa jukumu la ujenzi na kujenga chini ya Viwango,ujenzi wa muda mrefu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Aidha Bw,Makonda amewaonya watumishi wote wa mkoa wa dsm kuhakikisha wanatimiza majukumu yao waliyopewa na kuonya kuwa hata sita kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote wa mkoa iwapo hatawajibika katika kitengo au idara yake aliyopangiwa.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm